Burudani

Mduara wa Diamond na Khadija Kopa waingia kwenye Top 10 ya Radio ya Lagos, Nigeria

Diamond Platnumz kupitia wimbo wake ‘Nasema Nawe’ ametuthibitishia kuwa msanii wa Tanzania anaweza kufanya wimbo wenye mahadhi ya kwetu na bado ukapokelewa kwa ukubwa ule ule na mataifa mengine. Wimbo wake aliomshirikisha malkia wa Taarab, Khadija Kopa umeingia kwenye Top 10 ya Radio ya Nigeria.

kopa na diamond

‘Nasema Nawe’ imekamata namba saba kwenye African Top 10 ya The Beat 99.9 FM ya Lagos, Nigeria.

Mtanzania mwingine ambaye yuko kwenye chati hiyo ni Vanessa Mdee ambaye wimbo aliomshirikisha rapper K.O wa Afrika Kusini umeendelea kushika namba moja.

Hii inatoa somo kwa wasanii wetu kuwa sio lazima wasanii kufanya nyimbo zenye mahadhi ya Kinigeria au kutumia lugha ya kiingereza ili kuweza kufanya vizuri kwenye soko la kimataifa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents