Burudani

Miaka 10 ya Diamond, ni safari iliyojaa vikwazo, mitihani pamoja na mafunzo (Video)

Diamond Platnumz aka Simba anakwenda kufanya show yake ya nguvu nyumbani kwao Kigoma ikiwa ni sherehe ya miaka 10 ya safari yake kwenye muziki ambayo imejaa, vikwazo, majonzi, mitihani pamoja na furaha.

Twezetu Kigoma, 10 years of Diamond Platnumz ni safari ya Bata la kukata na shoka, kwani unaambiwa starehe za kila aina zitapatikana, watu watakunywa, kula, kucheza muziki pamoja mambo mengine ikiwa ni kujipongeza kwa kazi ngumu aliyoipitia katika safari yake ya muziki ambayo ilianza mwaka 2009.

FAHAMU MACHACHE USIYOYAJUA KUHUSU DIAMOND PLATNUMZ NA JINSI MAMA YAKE ALIVYOMPIGANIA

Jina lake halisi anaitwa Nasibu Abdul Juma maarufu kama “Diamond Platnumz”, alizaliwa tarehe 2, October mwaka 1989 katika Hospitali ya Amana Dar es salaam.

Mama yake alikuwa akimnunulia Diamond kanda za albumu za wasanii tofauti na kumuandikia baadhi ya nyimbo za wasanii hao ili mwanae aweze kuzishika na kuimba kirahisi, wakati mwingine hata kumpeleka katika matamasha tofauti tofauti ya talent show ili mwanae apate nafasi ya kuimba, kitu ambacho baadhi ya ndugu wa familia waliona ni kama kumpotosha na kumuharibu mtoto huyo badala ya kumuhimiza kimasomo.

“Nasikitikaga sana Wanapojaribu Kulinganisha Thamani yako kwangu na Mtu yoyote…Na kusahau kuwa pasipo wewe kunizaa na Kunilea kwa shida na tabu leo hii hakuna yoyote ambae angeniona wamaana….. Ikiwa wewe ndio Ulonifanya mie nikawa Duniani Basi you will always be My First priority then the rest will follow…Dharau na Manyanyaso Ulopitia kwenye kunilea Hakuna anayejua, Tabu na shida Ulizopitia kufanya hadi leo walau nionekane mtu mbele za watu.. eti mtu kirahisi tu anatokea na kukuringanisha na mtu… Mama MADALE is your House!!! na ikitokea kesho nimekufa pia NUSU ya Mali zangu zote ni zako.“ aliwahi kuandika Diamond Platnumz.

Aliongeza “Mwanao napambana usiku na Mchana Kwanza kwajili yako, Walau Ujifariji kwa Magumu Ulopitia kwa kunilea kwangu, i want you to Enjoy the life as Much as You can, Maana sina cha kukulipa zaidi ya Hicho..HAPPY BIRTHDAY MAMA I LOVE YOU SANA,“.

Baada ya Diamond kuonekana anapenda muziki mama yake alimsapoti kwa hali na Mali, miaka ya 2006-8 Queen Darleen alijitahidi kumshika mkono kaka yake kwa kumkutanisha na wasanii mbali mbali.

Miaka hiyo ya 2008 Diamond akawa anafanya Hip hop kuna nyimbo zilitoka za kurap kama Kiss To The Lady aliomshirikisha Mr Blue, kuna wimbo alishirikisha Hemedy PHD, Rommy Jons, pia kuna wimbo unaitwa Jisachi amemshirikisha Mabovu na Ngwair.

Mwaka 2009 Diamond aliachia wimbo ‘Kamwambie’ akiwa chini ya Bob Junior, wimbo huo alikuwa anamuimbia mwanamke aliyekuwa anampenda anaitwa Sarah Sadiki.

Taarifa zinadai kwa Mr Blue aliyempeleka Diamond Clouds Fm kutambulisha wimbo huo, ndipo Ruge aliposikia uwezo wa Diamond akaamua kumshika mkono na Kamwambie ikawa hit.

Mwaka 2014 alitoboa kimataifa na wimbo ‘My No1 Remix’ akiwa na Davido mpaka sasa anatikisa anga za muziki duniani ambapo kwaka huu muimbaji huyo ambaye ni rais wa label ya WCB ambayo imemiliki wasanii wakubwa ametajwa na CNN katika orodha ya wasanii bora 10 Afrika.

Wasanii aliowatengeneza na kuwa wakubwa kupitia label yake ya WCB ni Harmonize ambaye kwa sasa anajitegemea kupitia label yake ya Konde Gang, wengine ni Rayvanny, Mbosso, Queen Darleen pamoja na Lavalava ambao wapo chini ya WCB. Pia amewatengeneza mastaa wengi kupitia nafasi yake.

Diamond anamiliki media house, Wasafi Media ambayo kwa sasa inafanya vizuri. Hongera sana, Diamond Platnumz.

 

Miaka 10 ya Diamond, ni safari iliyojaa vikwazo, mitihani pamoja na huraha

Juhudi, pamoja support ya mama yake Bi Sadra.

2009 Nenda Kamwambie ilivyofungua milango.

Twezetu Kigoma, 10 years of Diamond Platnumz ni safari ya Bata la kukata na shoka, kwani unaambiwa starehe za kila aina zitapatikana, watu watakunywa, kula, kucheza muziki pamoja mambo mengine ikiwa ni kujipongeza kwa kazi ngumu aliyoipitia katika safari yake ya muziki ambayo ilianza mwaka 2009.

 

 

 

 

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents