Habari

Mitandao ya kijamii yalaumiwa kudhalilisha wanawake

Taasisi isiyo ya Kiserikali inayoundwa na Jumuiya za Wanawake wa Vyama vyote vya siasa (Ulingo) imelaani vitendo vya matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii vinavyofanywa na baadhi ya watu dhidi ya viongozi wanawake wana siasa pamoja na serikali kwa ujumla.


Mjumbe wa Sekretarieti toka Taasisi ya Ulingo wa Wanawake Bi. Saum Rashid akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wakitoa karipio juu udhalilishaji wa wanawake katika mitandao kwa kisingizio cha siasa, katikati ni Bi. Angelina Mutahiwa na kulia ni Bi. Dominata Rwechungura wajumbe wa Sekretarieti hiyo(PICHA MAELEZO)

Hayo yamesemwa leo Jijini Dar es Salaam na Mjumbe wa Sekretarieti ya Ulingo, Saum Rashid alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwaaajili ya kulaani watu wanaotumia mitandao ya kijamii kuwadhalilisha na kuwavunjia heshima viongozi wanawake.

“Matusi ambayo wanatupiwa na watu wasio na maadili ni matusi siyo kwa wahusika tu bali kwa wanawake wote, hivyo ikumbukwe kuwa hao wanaowalenga wanafamilia, watoto na marafiki na wanaongoza mamilioni ya watanzania,” alisema Bi. Saum.

Akizungumza bila kuwataja wanaotumia vibaya mitandao ya kijamii kudhalilisha viongozi, Bi.Saum alisema wanawake wanapodhalilishwa hasa na wanawake wenzao inawakatisha tamaa katika kutimiza majukumu yao hivyo akaomba mamlaka husika kusimamia Sheria ili mitandao isitumike vibaya.

Aidha Bi. Saum amesema kuwa anaamini viongozi wanawake ambao wamepewa heshima na dhamana ya kuongoza, wana uwezo mkubwa na wanastahili kuwa kwenye nafasi walizo nazo .

Taasisi hiyo ambayo inawashirikisha pia watu wenye ulemavu imelaani vikali vitendo vya udhalilishaji na kuwataka Watanzania warejee kwenye misingi ya utu na kuthaminiana kama maadili ya kitanzania yanavyoelekeza hasa kwa watoto wa kike.

Ulingo ni taasisi isiyo ya kiserikali inayoundwa na jumuiya za wanawake wa vyama vyote vya siasa vilivyosajiliwa kwenye na Msajili wa vyama vya siasa hapa nchini kwa lengo la kuwajengea uwezo wanawake katika nyanja mmbalimbali ili waingie kwenye vyombo vya maamuzi.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents