Burudani

Jay Moe adai hawezi kununua views YouTube

Mkongwe wa muziki Bongo, Jay Moe amedai kuwa hawezi kununua views katika mtandao wa YouTube kwani kufanya hivyo ni kujidanganya.


Rapper huyo ambaye kwa sasa anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Me and You’ amefunguka hayo kupitia The Playlist ya Times Fm na kueleza alishawahi kushawishiwa kufanya hivyo lakini hakukubali.

“No! no! ningekuwa tayari kufanya hivyo (ningefanya), mimi nimeshawishiwa na watu tangia Nisaidie kushare na hao watu hadi leo wananilaumu siunaona hadi leo hatujafika views milioni moja. Wananiambia we can do numbers kwenye mazingira haya na haya lakini mimi mwenyewe inaweza isiwe actual namba zangu, kwamba namba zangu halali ni hizi,” amesema Jay Moe.

Katika hatua nyingine msanii huyo amesema mitandao ya kijamii imesaidia sana wasanii wa sasa kukua na kujulikana, hata hivyo ameonya kuwa kama isingekuwepo kuna wasanii wasingesisikika na si kwa Tanzania pekee bali hata dunia nzima.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents