Habari

Serikali kujenga vyumba vya upasuaji 170

Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo ya jamii,Jinsia, Wazee na Watoto imejidhatiti kujenga vyumba vya upasuaji 170 kwa wajawazito ili kupunguza vifo vya mama wajawazito na watoto wachanga mpaka kufikia Juni 2018.

Akizungumza hayo wakati wa kupokea mashine ya kutoa dawa ya usingizi Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu alisema kuwa ujenzi wa vyumba hivyo vitasaidia kupunguza vifo vya wajawazito kwa asilimia 80  kufika 2025.

“Si tu vyumba vya upasuaji bali tutaimarisha mahitaji muhimu ikiwemo kujenga maabara ya damu,wadi za wazazi,tutanunua vifaa vyote vya upasuaji na kujenga nyumba moja ya watumishi wa afya kwenye kila kituoa cha kutolea huduma ya afya,” alisema Waziri Ummy.

Waziri Ummy amesema kuwa msaada wa mashine hiyo ya kutoa dawa ya usingizi kutoka Utepe Mweupe utaisaidia kupambana  kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga kwa asilimia 40 kufikia 2020 nchini.

Aidha Waziri Ummy amemuagiza Katibu Mkuu Wizara ya afya kuongeza wataalamu wa kutoa dawa ya usingizi wakati Serikali ipo katika mkakati wa kuongeza vifaa na dawa kwenye vituo vinavyotolea huduma ya afya hasa uzazi.

“Kama mpaka Juni mwakani tutakuwa tumemaliza hivyo Vyumba 170 vya upasuaji  wa kutoa watoto kwa wajawazito basi Katibu Mkuu na watendaji wako  mnatakiwa kuongeza wataalamu wa kutolea dawa ya usingizi wawili kila kituo kwa hiyo jumla wawe wataalamu 340” alisisitiza Waziri Ummy.

Kwa mujibu wa Waziri Ummy amesema kuwa Serikali imejiongeza kwa kutenga bilioni 8 kwa ajili kununua dawa za uzazi salama  ikiwemo dawa za kuzuia kifafa cha mimba,kuzuia mama kuvuja damu na hupatikana bila ya gharama yoyote.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents