Mitindo

Mitindo: Ifanye sketi yako kuwa gauni

Kila siku swala la mitindo linazidi kukua na kuimarika zaidi na ubunifu unazidi kuwa mkubwa kwa wabunifu, wanamitindo na hata watu wanaopenda kuonekana bomba zaidi.

Kwa kuzingatia hayo, baadhi ya wanamitindo nao wameonesha ubunifu wao kwa kuonyesha jinsi sketi inavyoweza kutumika kuvalika kama gauni na ukatokelezea bomba zaidi.

Ni muonekano mzuri endapo utatumia sketi iliyo ndefu zaidi kuifanya ionekane kama gauni, na hii inavutia sana ukiamua kuongeza manjonjo endapo rangi ya sketi sio ya kushtua sana au pia kwa rangi za kuvutia zaidi hupendeza kutokana na muonekano wake.

Dress sketi humependeza kila mtu, ila cha msingi ni kutambua aina ya sketi na mtindo wa gauni utakaobuni kwa skirt hiyo. Pamoja na kujua umbo lako likoje.

Na Laila Sued

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents