Habari

Serikali yatoa kauli kuhusu Uhuru wa Vyombo vya Habari

Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Harrison Mwakyembe amesema Tanzania inarekodi nzuri katika kuheshimu na kulinda uhuru vya habari miongoni mwa nchi za Afrika.

Akijibu hoja za Wabunge waliochangia Bajeti ya Wizara ya Habari kwa Mwaka wa fedha 2017/2018, Dkt Mwakyembe amesema hata utafiti uliofanywa kila mwaka na shirika la Waandishi wa Habari wasio na mipaka inaonyesha Tanzania imekuwa ikilinda uhuru huo wa vyombo vya habari.

“Kama ilivyo kila mwaka Tanzania inaongoza katika Jumuiya ya Afrika Mashariki katika nafasi ya 83 maana Kenya inatufuatia nafasi ya 95 pamoja na kwamba waandishi wengi wa Habari wanaotuma taarifa kuhusu ukandamizwaji. Sisemi kushikwa namba 83 basi tumefanikiwa sana habana hata kama tumezipiku nchi 107 duniani,” alisema Mwakyembe.

“Mimi ninachosema na naomba waheshimiwa wabunge mnielewe nasema laiti hawa reporters without borders wangekuwa wanafanya utafiti wao Kisayansi mimi naamini Tanzania tungekuwa tumeshika nafasi bora zaidi.”

Aidha Dkt Mwakyembe amesisitiza kuwa kauli zinazotolewa na baadhi ya watu kuwa Tanzania kuna ukandamizaji wa uhuru Vyombo vya Habari amesema si za kweli huku akisema serikali imekuwa ikihamasisha uundwaji vyombo hivyo.

Na Emmy Mwaipopo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents