Habari

Mke wa rapper Baghdad aachia wimbo, mfahamu zaidi

Muziki upo ndani ya familia ya rapper Baghdad. Mke wake, Gift ameachia wimbo wake wa kwanza uitwao Kadada.

DSC_0121

Gift Andrew Kabaka aka Jo Gift ni msanii ambaye alianza safari yake ya muziki akiwa katika kikundi cha Vipaji TZ chenye makazi yake Kigogo Mburahati, kikundi ambacho kinasimamiwa na muongozaji na mtayarishaji wa video mkongwe Adam Juma.

Amesema sasa yuko tayari kuianza safari yake rasmi akiwa amekamilisa mambo 3 makubwa, kwanza kupata mume ambaye ni msanii wa hip hop, Baghdad ambaye amemshirikisha kwenye wimbo wake huo uliotoka rasmi leo.

Ppili kuwa mke wa mtu na tatu na kubwa zaidi ni kuwa na mtoto wa kiume anayefahamika kwa jina la Kyl.

Jo Gift amesema hakugombana wala kuondoka kwa shari Vipaji bali alipopata nafasi ya kuwa voice artist wa kituo cha radio cha EFM, ndipo aliona anahitaji nafasi ya kutosha ili kuweza kuitendea haki kazi yake. Amesema Vipaji hawezi kupasahau kwa kuwa ndipo palipomkutanisha na mume wake.

Aidha amesema kuwa mwaka jana ulikuwa mwaka wa kuvuna na kutimiza malengo yake ya kufunga ndoa ambayo alifunga July 25 na pia mwaka 2015 alibarikiwa kupata mtoto.

“Mume wangu namshukuru sana kwa kuwa amekuwa mume bora na mfano kwangu na kusema ukweli najihisi ni wa gharama kama nilivyoimba kwenye wimbo wangu huo,” amesema.

Jo Gift amesema wimbo wake umefanyika katika studio za Vipaji TZ, producer akiwa ni Abbah Process na wimbo umeandikwa na Baghdad, kila kitu hadi melody. Amewashirikisha Baghdad na Dream.
“Ili kuupata kwa wanaohitaji waandike neno kadada watume kwenda 0652894871.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents