Michezo

Mkhitaryan amshukuru Jurgen Klop

Mchezaji wa klabu ya Manchester United, Henrikh Mkhitaryan amemshukuru sana kocha wake wazamani Jurgen Klop kwa
ushauri wake uliomsaidia kuimarika katika timu yake mpya uwanja wa Old Trafford.

Kocha huyo wa Liverpool alimshauri mchezaji huyo wakati mgumu walipokuwa katika klabu ya Borussia Dortmund 2013.

Mapema msimu huu Mkhitaryan mwenye umri wa miaka 28 hakucheza kwa muda wa wiki 10 na kukumbuka ushauri aliopewa na Klopp.

”Namshakuru sana Klopp”, alinisaidia kiakili”, aliambia BBC.

Raia huyo wa Armenia alihudumu miaka miwili akimchezea Klopp ambaye alijiunga na Liverpool 2015.

“Nilipokuwa Dortmund, nilikuwa na shikinizo kubwa la kiakili baada ya kushiriki mechi chache ambapo tulikuwa hatuchezi vyema ,aliongezea Mkhitaryan, ambaye amefunga mara tano msimu huu.

”Klopp alinionyesha njia, alinisaidia na kunambia kutovunjika moyo kwa kuwa ufanisi mkubwa ulikuwa unakuja. Alinisaidia kuwa mchezaji nilivyo”.

Source: BBC

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents