Michezo

MO Ibrahim wa Simba SC arejea mazoezini kuivaa Azam FC

Kocha wa klabu ya Simba SC, Joseph Omog amesema kuwa mshambuliaji Mohammed Ibrahim ameanza mazoezi kuelekea mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya Azam FC.

Kocha Omog ameongea na mtandao wa Goal, MO ameanza mazoezi mepesi nimejisikia faraja moyoni licha ya kutokuwa na uhakika kama atakuwa fiti kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi au vinginevyo.

“Ukweli nimefurahi kumuona kwenye mazoezi leo amenifanya nipate matumaini, kwasababu ni mchezaji ambaye anamchango mkubwa kwenye kikosi chetu kukosekana kwake nipigo kwetu ingawa wapo watu wa kucheza nafasi yake,”amesema Omog.

Kwaupande wake Daktari wa Simba Yasini Gembe, amesema wataendelea kufatilia hali ya mchezaji huyo kwa karibu hadi kufikia siku ya mchezo Jumamosi.

Gembe amesema wanatambua umuhimu wa mchezaji huyo na ukubwa wa mchezo unao wakabili hivyo yeye kwa kushirikiana na wenzake watapambana ili kuona MO, anakuwepo uwanjani siku hiyo.

Daktari huyo amesema wanatambua umuhimu wa ushindi katika mchezo huo hivyo mashabiki wa Simba wasiwe na hofu watajitahidi kulirekebisha hilo na kumfanya mchezaji huyo aweze kuipigania timu yake siku ya mchezo Jumamosi

“Imani yetu ni kuhakikisha anakuwepo kwenye idadi ya wachezaji ambao watatumika kwenye mchezo huo najua kocha ndiyo mwenye maamuzi ya kutumia mchezaji amtakaye lakini kazi yetu kama madaktari ni kuona kila mchezaji wa Simba aliyokuwa mgonjwa anapata huduma na kuwa sawa kwa ajili ya kuipigania timu yetu,”amesema Gembe.

Mo ambaye alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya kifundo cha mgu aliumia kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar kwenye mchezo wa nusu fainali dhidi ya Yanga baada ya kugongana na mlinzi Hajji Mwinyi.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents