Michezo

Morrison alivyowajibu Yanga kuhusu kwenda FIFA 

Baada ya Mwenyekiti wa Yanga Dkt. Mshindo Msolla kudai kuwa Jumatatu, Agosti 25 wanapeleka malalamiko yao rasmi FIFA juu ya utata wa mkataba wa winga Bernard Morrison, winga huyo ameibuka na kuwajibu.

Image

Mwenyekiti wa Yanga, Dkt. Msolla, Morrison na wachezaji wenzake wa Simba

Mwamba huyo kutoka nchini Ghana, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram amewapiga kijembe waajiri wake wa zamani Yanga kwa kuweka picha akiwa na Kiungo Jonas Mkude inayoonyesha wanacheka, kisha akaandika kwa namna alivyosikia taarifa za kesi yake kufikishwa CAS na FIFA.

https://www.instagram.com/p/CEOMnmzguyO/

Morrison jana alionyesha thamani yake kwa kufunga bao pamoja na kutoa asisti kwenye ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Vital’o ukiwa ni mchezo wa Simba Day.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga Dkt Mshindo Msola alisema jana kuwa imemjumuisha Morrison kwenye usajili wao, jina lake wakiwa wamelisajili kwenye mfumo wa FIFA (TMS) kwa kuwa bado ni mali yao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents