Habari

Maandamano makubwa yatarajiwa Belarus, Rais aamuru jeshi kulinda nchi

Maandamano makubwa yanatarajiwa kufanyika hii leo nchini Belarus dhidi ya rais Alexander Lukashenko, ambae tayari ameliamuru jeshi kuendelea kuilinda nchi baada ya waandamanaji kupinga matokeo yaliompa ushindi wa asilimia 80 katika uchaguzi uliofanyika mapema mwezi huu.

Belarus | Proteste gegen Präsident Lukaschenko (Reuters/V. Fedosenko)

Wakosoaji wa kiongozi huyo wa muda mrefu barani Ulaya, wamepanga migomo na maandamano makubwa ambayo hayajawahi kuonekana katika historia ya taifa hilo la zamani la Umoja wa kisovieti, kupinga kuchaguliwa tena kwa Lukashenko kama rais wa nchi hiyo na kumtaka aondoke madarakani.

Juma lililopita zaidi ya watu lakini moja waliandamana kote nchini Belarus. Kiongozi wa upinzani aliye uhamishoni katika nchi jirani ya Lithuania Svetlana Tikha-novs-kaya ameliambia shirika la habari la AFP kwamba waandamanaji wanaodai demokrasia ni lazima wapambane kupata haki yao na wasibabaishwe na madai ya Lukashenko, kwamba nchi iko chini ya kitisho cha kijeshi.

Amesema waandamani ni watu wa Belarus na walio wengi na kamwe hawatoondoka hadi matakwa yao yatimizwe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents