Habari

Rais Magufuli aendesha harambee ya Ujenzi wa Msikiti wa Chamwino

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli, ameendesha harambee ya kuchangia ujenzi wa Msikiti wa Chamwino katika Misa Takatifu na uzinduzi wa Kanisa, Parokia ya Bikira Maria Imakulata, Ikulu Chamwino Mkoani Dodoma. Zaidi ya shilingi milioni 48 ziliipatikana pamoja na ahadi za vifaa vya Ujenzi.

Single News | Ruvuma Region

Harambee hiyo ameifanya hii leo Agosti 23, 2020, yenye lengo la kuhakikisha Makao Makuu ya nchi yanakuwa ni sehemu ambayo imezungukwa na uwepo wa Mungu, na kueleza kuwa Msikiti wa Chamwino bado ni mdogo hivyo ipo haja ya kuchangia ili uweze kuwa mkubwa.

“Mahali ambapo ni Makao Makuu ni lazima pazungukwe na watu wanaomtukuza Mungu, Baba Askofu kama utaniruhusu na hili nakuomba sana, basi tutumie siku ya leo pia tuchange tuanze kujenga Msikiti wa ndugu zetu Waislamu ambao Msikiti wao ni mdogo na wapo pale kwa ajili ya kumtukuza Mungu na baadhi ya wasaidizi wangu ni Waislamu na yupo anaitwa Alhaji na ameshaenda kuhiji”, amesema Rais Magufuli.

Aidha Rais Magufuli ameongeza kuwa, “Tutamuomba Baba Paroko angalau akaziwasilishwe kwa Sheikh kwenye Msikiti wetu na tutajipanga taratibu namna ya kuanza kuukarabati, tukimaliza tutaendelea tena kwenye Kanisa lingine ili utukufu wa Chamwino katika kumtukuza Mungu ukasimame katika maisha yote, sasa Baba Askofu naangalia angalia kikapu hapa, umeniruhusu aahaa”.

Katika harambee hiyo aliyoifanya Rais Magufuli, amekusanya kiasi cha zaidi ya Shilingi Milioni 48, ambapo pia imetolewa mifuko ya Saruji pamoja na michanga.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents