Michezo

Mourinho aamuru kabati la vifaa la Alexis Shanchez kuhamishwa

Meneje wa Manchester United, Jose Mourinho ameamuru kabati la kuhifadhia vifaa na jezi la mchezaji wake mpya, Alexis Shanchez lihamishwe kutoka lilipokuwa awali na kuwekwa karibu na kinda wa timu hiyo mwenye umri wa miaka 19, Marcus Rashford katika chumba cha kubadilishia nguo ndani ya United.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Chile alimaliza uhamisho wake wa kutua  Old Trafford siku ya Jumatatu ya juma lililopita katika dili ambalo limefanya Henrikh Mkhitaryan kutoka katika timu hiyo na kujiunga na Arsenal.

Kwa mujibu wa mtandao wa The Sun umesema kuwa kitendo kilichofanywa na Mourinho ni katika kuhakikisha Sanchez anakuwa karibu na Rashford ili kumpatia uzoefu ndani na nje ya uwanja.

Habari kutoka ndani ya Old Trafford zinasema ni kawaida kwa meneja huyo kuwachanganya wachezaji wenye umri tofauti ili kubadilishana uzoefu hivyo Sanchez ataweza kumuweka Rashford katika hatua nyingine kisoka soka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents