Burudani

T.Touch amkingia kifua Young Dee

Producer Mr T Touch amesema ufanyaji kazi wake na Young Dee ni wa kawaida na si kama watu wanavyomchukulia msanii huyo kutokana na kuwa na historia ya kubadili management kila wakati.

Mr T Touch

Mr T Touch amesema kitu kikubwa ambacho wanafanya wao kama Touch Sound ni kujaribu kumtengenezea mazingira tofauti Young Dee na kule alipokuwa awali.

“Unajua sometime pia mtu anaweza kuwa na mambo mengi kutokana na mazingira ambayo yeye amekuwepo labda hajapata mtu wa kumsimamia vizuri.

“Hata home watoto wanaweza kuwa hata watatu au wanne alafu wakawa na tabia tofauti lakini mzazi akataka kuwatreat wale wote in the same way ambayo anafikiria kwake itakuwa sahihi, lakini siyo sahihi katika wale watoto watatu kwa sababu kila mmoja ana tabia yake na mzazi anatakiwa ajua namna ya kudeal na kila mmoja,” alisema Mr T Touch.

Aliongeza kuwa kwa sasa kikubwa wanachoangalia kwa Young Dee ni kipaji chake na namna ya kukiendeleza na namna ya kumtumia katika kazi zaidi.

“Tumezaliwa kufanya hivi ambavyo tunavifanya kwa sababu ndivyo tulivyochagua na kila kazi ina changamoto yake lakini usipokubaliana na changamoto ya kazi yako ni vigumu kusonga mbele kwa sababu kitu kidogo kinapotokea kinakuvuruga, kikija kikubwa zaidi ya kile unashindwa kukabaliana nacho,” alisema na kuongeza.

“Pia itapunguza uwezo wa kufanya kazi, mimi muda wote huwa naaangali ni kitu gani kinaweza kunifanya kusonga mbele,” Mr T Touch alikiambia kipindi cha Ladha 3600.

By Peter Akaro

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents