Burudani

Mrisho Mpoto amliza Vanessa Mdee…lakini si kwa ubaya!

Sio kila siku unaweza kuamka na furaha na kila kitu kikawa sawa. Kuna nyakati ambazo mtu unaweza kujikuta hauko vizuri kutokana na baadhi ya mambo yako kukwama.

mpoto n vee

Katika hali kama hii binadamu huhitaji kitu kidogo tu kama maneno ya kutia moyo kutoka kwa mtu unayemuheshimu, ambayo yanaweza kuirudisha furaha iliyokuwa imepotea kwa muda.

Ujumbe wa pongezi kwa muimbaji wa ‘Never Ever’ Vanessa Mdee umegeuka kuwa faraja kwa Vee Money ambaye kwa mujibu wa post yake ya Instagram siku ya leo Dec 8 haikuanza vizuri baada ya baadhi ya mambo yake kukwama.

Mpoto Vee

Vanessa ambaye yuko Nigeria amepost screenshot (hapo juu) ya post ya wiki tatu zilizopita aliyopongezwa na Mpoto kwa ushindi wa tuzo ya Afrima. Vee Money ameisindikiza kwa caption hii:

“Siku yangu leo haija anza vizuri kuna mambo hayaendi. Na yananikata sana – huwezi amini ni jinsi gani nilikuwa nahitaji kusoma message yako. Mungu akubariki. Hadi machozi yananitoka anyway @mrishompoto Asante Sana”

Vanessa pia amepost Marimba Chart ya Bongo5 ambayo wiki hii amekamata nafasi ya kwanza na kuandika;

“Even on Bad Days. Gods always showing you signs. Just look out for them. #NeverEver Game . #MyTeamAndI #MnyooshoWaNahreel”

vee marimbaa

Pole sana Vanessa kwa chochote kilichokuharibia siku yako leo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents