Burudani

Mtoto wa Lil Wayne, Reginae Carter asema baba yake anaendelea vizuri

Mwanamuziki wa hiphop nchini Marekani Dwayne Michael Carter Jr maarufu kama Lil Wayne juzi alikimbizwa hospitali baada ya kukutwa hotelini akiwa hajitambui.

Baada ya kufanyiwa matibabu watu wa karibu wa rapa huyo mwenye umri wa miaka 34 walitaka kumtoa hospitali ili aweze kufanya onyesho mjini Las Vegas lakini madaktari walimshauri Wyne apumzike na asipande ndege katika kipindi hiki.

Binti wa Lil Wyne ambaye ni mtoto wake wa kwanza Reginae Carter amewatoa hofu mashabiki duniani kote waliokuwa na wasi wasi juu ya maendeleo ya afya ya Lil Wayne baada ya kuandika ujumbe kwenye mtandao wa Tweeter unaoashiria hali ya baba yake kuwa nzuri.

”Baba yangu anaendelea vizuri nashukuru kwa kila aliyeguswa, usiamini kila unachokisikia” aliandika Reginae Carter.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents