Burudani

Mtoto wa Madonna, David Banda (8) ndiye aliyemchagulia vazi la kuvaa kwenye tuzo za Grammy

Mwimbaji Madonna aliwasili katika tukio la ugawaji wa tuzo za Grammy lililofanyika Jumapili (January 26) huko Los Angeles, Marekani akiwa na mtoto wake wa kiume David Banda, wote wakiwa wamevaa suti nyeusi.

madonna n david

Madonna alimwambia mtangazaji wa Red Carpet Ryan Seacrest kuwa suti ya Ralph Lauren aliyovaa usiku huo ni uchaguzi wa mwanaye David Banda mwenye miaka 8 aliyetaka wavae nguo zilizofanana.

madonna n david2

Seacrests alipomuuliza Banda kama mama yake huwa anamskiliza ushauri wake katika swala la fashion, mtoto huyo alijibu “Yes, very well.”

Madonna alimuasili David Banda kutoka Malawi mwaka 2006.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents