Michezo

Muzamiru Yassin agombaniwa na klabu za Afrika Kusini

Kiungo wa klabu ya Simba SC, Muzamiru Yassin amekuwa almasi kwa baadhi ya timu za Afrika Kusini.

Kiungo wa klabu ya Simba , Muzamiru Yassin

 

Muzamiru yuko Afrika Kusini akiitumikia timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) katika michuano ya Cosafa ambayo imetinga nusu fainali kwa kuwatoa wenyeji Afrika Kusini hatua ya robo fainali.

Taarifa zinaeleza, mawakala kadhaa wameanza kumfuatilia kwa karibu baada ya kuwa mmoja wa wachezaji waliofanya vizuri zaidi katika michuano.

Baadhi ya magazeti ya Afrika Kusini yameeleza kuwa nyota huyo wa Simba na timu ya taifa amekuwa lulu kutokana na uwezo aliyo uonyesha katika mechi zote ambazo Stars imecheza.

Imeelezwa miongoni mwa timu zilizovutiwa ni Bidvest na Mpumalanga Black Ace lakini wataalamu wanaofuatilia wachezaji(mawakala) wanaweza kuwapeleka wachezaji hata katika timu za nje ya Afrika Kusini.

Katika michuano hiyo Muzamiru amekuwa injini kuu ya kuendesha kiungo cha Stars na kusababisha mvuto mkubwa kwa watazamaji.

By Hamza fumo

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents