Burudani

Mwana FA kwenda Afrika Kusini kushoot video ya wimbo mpya

Mwana Fa ni miongoni mwa wasanii waliositisha kazi zao za muziki ili kupisha mambo ya kampeni pamoja na uchaguzi, na sasa baada ya hayo yote kumalizika yuko tayari kurejea kwenye uwanja wake wa kujidai, yaani muziki.

FA

Binamu amesema kuwa ana kazi nyingi ambazo amezifanya na anaendelea kufanya zingine, “Kweli nina kazi wala sio kazi moja wala sio kazi mbili, yani nina kazi kadhaa na wiki ijayo narekodi nyingine,” aliiambia Planet Bongo ya East Africa Radio. “ lakini haya mambo ya uchaguzi kila kitu kilikuwa Magufuli, Lowasa, kwa hiyo ikawa ngumu kidogo kutoa ngoma, watu hype ya uchaguzi ilikuwa kubwa sana.”

Rapper huyo pia amebainisha kuwa sasa yupo tayari kuachia wimbo mpya, na video ya wimbo huo anaenda kuifanyia video AFrika Kusini weekend hii. “lakini now kwamba uchaguzi umekwisha tunataka kutoa ngoma na wikiendi hii naenda kufanya video South Africa.” Alisema FA.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents