Michezo
Nassor Idrissa arithi mikoba ya Said Mohamed Abeid, Azam FC
Aliyekuwa makamu Mwenyekiti wa Klabu ya Azam FC, Nassor Idrissa ameteuliwa kuwa Mwenyekiti mpya wa timu hiyo akirithi mikoba ya Alhaji Said Mohamed Abeid, aliyefariki dunia mwanzoni mwa mwezi huu.
Nassor Idrissa
Kwa mujibu wa barua iliyoandikwa na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba, na kuituma kwenda kwenye Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuwafahamisha mabadiliko hayo, imeeleza kuwa Shani Christoms Mligo, ndiye atakuwa Makamu Mwenyekiti mpya wa timu hiyo akichukua nafasi ya Idrissa.
Mabadiliko hayo ya kiuongozi yamefanywa na Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC, ambapo uteuzi huo umeanza rasmi Novemba 29 mwaka huu.