Burudani

Navy Kenzo na Patoranking katika spika zako ‘soon’

Kundi la muziki linalofanya vizuri na wimbo wake Game, Navy Kenzo, limesema lipo kwenye maandalizi ya mwisho ya kufanya kolabo na msanii wa Nigeria, Patoraking.

Navykenzo

Mmoja wa wasanii wanaounda kundi hilo, Aika ameiambia Bongo5 kuwa kila kitu kiko poa.

“Kila kitu kinaenda sawa, sasa hivi tunajipanga kufanya kolabo na Patoranking,” amesema. “Pia kuna msanii mmoja wa nje ambaye alitutumia ngoma anaitwa Jizzy anataka tufanye remix ya wimbo wake, original alifanya na Ice Prince. Kwahiyo mashabiki wakae mkao wa mambo mazuri.”

Navy wamedai kuwa mwaka 2015 ulikuwa na mafanikio kwao.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents