Burudani

Ngoma zangu zinadumu zaidi – Mo Music

Mo Music anaamini kuwa muziki wake unadumu zaidi masikioni mwa watu na ndio maana haangalii watu wanasema nini bali anangalia wanataka nini.

11849116_1506629606295702_1754705394_n

Mo ameiambia Bongo5 kuwa ili kuelewa muziki wake unahitajika kuusikiliza kwa makini kabla ya kutoa maoni.

“Kwanza nashukuru Mungu mpaka sasa kazi yangu inaenda poa sana. Mo Music ni msanii wa muziki wa peke yake, ni msanii anayehitaji subira sana ili uweze kujudge,” amesema.

“Obvious mimi siangaliagi watu wanasema nini, naangalia wanataka nini. Ukiweza kulijua hilo kwenye soko lako la biashara ni jambo jema kwa sababu unaweza ukaitambulisha biashara yako ambayo inaweza kuwa kubwa leo halafu kesho ikapotea kabisa. Lakini biashara nzuri ni ile yenye maisha marefu, ndio muziki wangu ulivyo. Nikitoa ngoma leo itaonekana ya kawaida lakini kadri siku zinavyozidi kwenda ndipo zinapozidi kufanya vizuri.”

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents