Burudani

Ni mara ya 10 Majuto anazushiwa kifo, tunaumia sana – Hamza Majuto

Hii ni mara ya  10 muigizaji mkongwe wa filamu, Mzee Majuto anazushiwa kifo katika mitandao ya kijamii kwa mujibu wa mtoto wake, Hamza Majuto.

Familia yake imeiomba serikali na vyombo husika ikiwemo mamlaka ya mawasiliano, kuwachukulia hatua watu wanaozusha taarifa za kifo baada ya jana usiku kuanza kusambazwa uzushi wa namna hiyo tena.

Akiongea katika kipidi cha SUPAMIX kinachorushwa na East Africa Radio, mtoto wa Mzee Majuto, Hamza Majuto amesema kuwa kama familia wameziona taarifa hizo kwenye mitandao ya kijamii na wala hawafahamu nia ya watu hao wanaozusha taarifa za kifo cha baba yake mara kwa mara.

Aidha mtoto huyo wa Mzee Majuto amesema kwamba baba yake kwa sasa anaendelea vizuri tangu aliporudi kutoka nje ya nchi na sasa (Majuto) yupo kwenye mapumziko kama jinsi ambayo inatakiwa.

“Tangu jana nimepokea simu na sms zaidi ya 500 zikitaka nithibitishe kuhusu kifo cha mzee. Kiukweli hii ni mara ya 10 kwa mzee kuzushiwa taarifa ya kifo. Natambua kwamba kuna vyombo vya usalama pamoja na mamlaka inayohusika na makosa ya mitandao hivyo hili la kuzusha kifo ni kosa la jinai naiomba basi TCRA ifuatilie ili kujua dhamira ya huyu mtu ambaye amekuwa akizusha taarifa za kifo” amesema Hamza.

Hata hivyo, Kijana huyo amesema kwamba kwa sasa wapo mapumzikoni lakini hawawezi kusema ni wapi kwa ajili ya kuepusha usumbufu ili kumsaidia mzee Majuto apate mapumziko mazuri.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents