Michezo

Kwa rekodi hizi nani usiku wa leo ‘atapata tabu sana’ kwenye mchezo kati ya Argentina na Nigeria

Wakati dunia nzima ikisubiria mchezo wa kukata na shoka wa Kombe la Dunia kati ya Argentina na Nigeria, tuangalie rekodi za timu zote mbili kabla ya mchezo wa leo usiku.

Timu zote mbili zimekutana mara nne kwenye michuano ya kombe la Dunia ya mwaka 1994, 2002, 2010 na kombe la Dunia la mwaka 2014 nchini Brazil .

Kwenye mechi zote nne Argentina wameshinda mechi zote lakini hakuna magoli mengi kwenye mechi zao yaani matokeo yake huwa ni tofauti ya goli moja.

1994: Nigeria 1-2 Argentina

2002: Nigeria 0-1 Argentina

2010: Nigeria 0-1 Argentina

2014: Nigeria 2-3 Argentina

Rekodi hii ni ya michezo ya Kombe la Dunia pekee na kwa upande wa mechi za kirafiki, timu hizo zimekutana mara tatu na Nigeria imeshinda mechi mbili na kupata sare mchezo mmoja.

Kikubwa zaidi usiku wa leo ni kwamba Argentina watahitaji ushindi kwa namna yoyote ileĀ  waweze kusonga hatua ya 16 bora ya michuano hiyo.

Je, unadhani Nigeria itawatoa kimaso maso waafrika kwenye mchezo huo na kuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kusonga mbele kwenye michuano ya Kombe la Dunia 2018?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents