Burudani

Nicki Minaj avunja rekodi nyingine kwenye chati za Billboard

Single ya Nicki Minaj ’Only’ imefanikiwa kukamata nafasi ya kwanza kwenye Hot R&B/Hip-Hop Songs chart za Billboard, na kumfanya awe msanii wa kike aliyewahi kuwa na nyimbo nyingi zaidi zilizofika nafasi ya kwanza tokea chati hizo zianzishwe miaka 56 iliyopita.

nicki-minaj-v-magazine-4-1415210222

Nicki amevunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Missy Elliot aliyekuwa na nyimbo tatu zilizokamata nafasi ya kwanza kwenye Billboard, huku Minaj sasa akiwa amefikisha nyimbo nne.

Da Brat na Iggy Azalea ambao wote wana nyimbo mbili zilizofanikiwa kukamata nafasi ya kwanza wanakamilisha idadi ya wasanii wa kike waliofanikiwa kuwa na nyimbo nyingi kwenye nafasi ya kwanza kwenye chati za Billboard.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents