Nilikuwa fundi majiko mzuri

Nilikuwa fundi majiko mzuri
Miongoni mwa wasanii wachache wa muziki wa Bongo Flava ambao hawafichi
dili walizowahi kupiga kabla hawajatoka kunako game ni pamoja na
Mohamed Ally a.k.a Z-Anto ambaye hivi karibuni alitamka kwamba, yeye ni
fundi mzuri wa kutengeneza majiko


Akipiga stori ndani ya kipindi cha ‘Nani ni nani’ kilichoasisiwa na Frank Mtao na kurushwa hewani kupitia Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, msanii huyo anayeunda familia ya Tip Top Connection alisema kwamba kabla hajatoka kupitia muziki alikuwa akipiga dili mbalimbali za sanaa ikiwemo hiyo ya kutengeneza majiko.

“Nakumbuka siku moja nilipokuwa Nairobi kwenye shoo, nilikatiza kwenye mtaa fulani nikakuta kuna sehemu watu wanatengeneza majiko kwa kutumia mabati magumu, nikavutiwa ikabidi niwaombe nijaribu. Huwezi kuamini, nilitengeneza jiko zuri mpaka wakabaki wanashangaa kwasababu walidhani mimi ni muziki tu,” alisema Z-Anto ambaye hivi karibuni atadondosha video ya wimbo wake mpya, ‘Peace & Love’ aliyowashirikisha Pingu na Juacali kutoka Kenya.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents