Bongo5 ExclusivesBongo5 MakalaBurudaniHabariLifestyleMakalaMichezo

Nini siri ya mastaa wengi duniani kutumia likizo zao Afrika ?

Wachezaji wakubwa duniani wabadilisha upepo kwenye holiday zao na kuzihamishia Afrika, kitu gani kinawavutia zaidi kuja kwenye mapumziko katika bara la Afrika ? kitu gani kipo nyuma ya pazia ?

Miaka ya nyuma tulishazoea kuwaona wachezaji na mastaa mbalimbali wakubwa duniani wakienda kwenye holiday zao kwenye mataifa makubwa ambayo yameendeleza zaidi duniani mfano. Marekani hasa katika jimbo la miami ingawa mpaka sasa mastaa wanaenda sana tu.

sehemu zingine ni falme za kiarabu barani Asia maeneo kama Bali na sehemu nyinginezo za kutalii pia Ugiriki, maeneo kama Santorini, Mykonos na Athens bila kusahau Amerika maeneo kama Brazil Jmaica na mengineyo mengi.

 

Miaka ya hivi karibuni tumeanza kuwaona mastaa wengi duniani wakibadili upepo na kuanza kuja barani Afrika hasa taifa kama Tanzania ambapo wengi wanaenda Zanzibar, Ngorongoro, Mlima kilimanjaro.

Tumeshaowana mastaa wengi kama David Beckham, Idris Alba, Will Smith, Mamadou Sakho na wengine lakini kwa sasa mastaa ambao wapo Tanzania ni Ander Herrera kutoka Uhispani anayekipiga katika klabu ya PSG lakini mwenzake kutoka PSG raia wa Argentina Mauro Icard pia beki wa Inter Milan ya Italia na raia wa Uholanzi Stefan De Vriji.

Mbali na hao wengine ni beki wa Liverpool na raia wa Ufaransa Ibrahima Konate, Mich Batshuayi streka wa chelsea na timu ya taifa ya Ubelgiji.

Mbali na Tanzania wengi wanajua kuwa aliyekuwa kiungo wa Mna United raia wa Ufaransa Paul Pogba anatumia likizo yake nchini Guinea.

Mbappe wa PSG, N’Golo Kante wa Chelsea, Riyad Mahrez wa Man City, Camavinga wa Real Madrid, Dembele wa Barcelona, Slimani, Bennacer na Benrahma wanatumia likizo zao nchini Morocco.

Kocha wa Roma ya Italia Jose Mourinho anatumia likizo yake nchini Namibia, Kai Havertz wa Chelsea nraia wa Ujerumani anatumia likizo yake nchini Afrika Kusini.

Mauro Icardi, Ander Herrera, Ibrahima Konate na Stefan de Vrij wanatumia likizo zao nchini Tanzania.

Memphis Depay wa Barcelona raia wa Uholanzi na Quincy Promes wanatumia likizo zao nchini Ghana. Samuel Umtiti na Aurélien Tchouaméni wanatumia likizo zao nchini Cameroon.

Wengi wanahisi kwa wale wachezaji wenye asili ya Afrika huenda wamekuja kwa sababu ni asili ya mataifa yao lakini kuna wachezaji wengi na mastaa wengi wanakuja na sio asili ya Mwafrika.

Unahisi ni kitu gani kinawavutia hawa mastaa? Afrika tumeanza kuvitangaza vivutio vyetu vilivyo au wao wameona waje kwa ajili ya kupumzika tu na kulifahamu bara la Afrika vilivyo ?

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents