Burudani

Nisher atayarisha ngoma mpya ya Fid Q ‘Bendera ya Chuma’

Nisher ni mtu mwenye vipaji vingi.

Zaidi ya kuongoza video (kitu kilichompa umaarufu zaidi), Nisher pia ni muimbaji mzuri wa R&B na mtayarishaji wa nyimbo na zote anavifanya katika level ya ‘upro’.

Hivi karibuni ametayarisha wimbo mpya wa Fid Q uitwao ‘Bendera ya Chuma’.

“Nimeproduce kila kitu, music, everything nikamtumia akapenda. Nimemtupia catalogue ya nyimbo zangu kama 15 akaangalia akapenda akasema ‘we mtoto sikuwezi,” amesema Nisher.

“Nimemtumia AY kasikiliza akasema ‘Nisher huyu, huyu wa mavideo’. Kwahiyo AY pia yupo onboard so nataka nimtengenezee pia ngoma kadhaa. Na hopefully kuanzia hapo itaanza kwenda kama explosion sasa. Utagundua kwamba hicho labda ndio kitakuwa kikubwa zaidi, mi sijui.”

Nisher pia ndiye atakayeongoza video ya ngoma ya Fid Q, Bongo Hip Hop.

Related Articles

Leave a Reply

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents