Michezo

Pacome na Aucho watakichafua sana Ijumaa – Miguel Gamond

kocha wa Mabingwa hao wa Tanzania Young Africans Miguel Gamondi ametamka kwamba kuna uwezekano mkubwa Pacome Zouzoua na Khalid Aucho wakafanya kazi kubwa kwenye mechi ya Ijumaa.

“Tunaweza kuwa na kikosi chenye mabadiliko ni sisi tutaamua tucheze vipi na tuanze na nani kwani wale waliocheza mechi iliyopita wako sawasawa lakini pia wale ambao walikuwa na shida ya afya baadhi wamekaa sawasawa.

“Aucho (Khalid) yuko kwenye nafasi kubwa ya kucheza kuliko wenzake naweza kusema asilimia themanini, Pacome naye amerejea anafuatia nyuma ya Aucho kuhusu Yao amekuja lakini tutaamua hukuhuku cha kufanya,” alisema Gamondi.

Yanga inahitaji sare yoyote ya mabao au ushindi kwenye mchezo huo ili itinge nusu fainali ya mashindano hayo ikiwa ni rekodi kutokana haikuwahi kucheza hatua hiyo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents