Habari

Picha: Diamond amtambulisha King Maru aliyepiga Saxophone katika ‘My Number 1’ na ‘Tupogo’ ya Ommy Dimpoz

Inawezekana wewe ni mpenzi wa nyimbo za mastaa wanaozitawala chart za Marimba Ommy Dimpoz katika nafasi ya kwanza na Diamond Platnmuz katika nafasi ya pili, lakini pamoja na kupenda single zao ambazo ni hit kwa sasa kuna uwezekano ukawa hujapata bahati ya kumuona au kumfahamu mtu aliytepiga Saxophone katika nyimbo hizo.

diamond

Diamond Platnumz ameamua kumtambulisha kwa mashabiki King Maru, mtu aliye nyuma ya kionjo kitamu kilichoipendezesha zaidi ‘My Number One’ ya Platnumz pamoja na ‘Tupogo’ ya Ommy Dimpoz.

King Maru-2
King Maru

Kupitia blog yake ya This is Diamond, ameweka picha za King Maru walipokuwa studio wiki iliyopita wakirekodi remix ya ‘My Number One’ aliyomshirikisha Davido wa Nigeria. Hiki ndicho alichokiandika star huyo kwa ‘Kesho’ sambamba na picha hizo:

“Anafahamika kama Mzee King Maru, mwenyewe anapenda kujiita,mtu gani huyu..ni mmoja ya wazee ninaowaheshimu sana kwenye tasnia yetu ya mziki..ana husika zaidi na upigaji wsa chombo cha muziki ambacho naamini ndiyo chombo kigumu zaidi kukitumia,SAXOPHONE ama mdomo wa bata. kama hufahamu amefanya kazi na wasanii wengi wa Bongo fleva ambapo,SAXOPHONE yake inasikika Barnaba,Rinnah na wengineo na kama ulikuwa hufahamu zaidi Mzee Maru amefannyama wakeya kwenye nyimbo ya mwanangu Ommy Dimpoz,tupogo na SAXOPHONE unayoiskia kwenye wimbo wangu wa Number one ni mzee Maru mwenyewe…tegemea kuskia akifanya yake ndani ya Number one 2 niliyofanya na Davido” Ameandika Diamond

King Maru-1

Toka mastaa hao wa bongo flava na maswahiba Ommy Dimpoz pamoja na Diamond Platnumz watoe single zao ambazo kwasasa ni hits ndani na nje ya Tanzania, King Maru amegeuka kuwa dhahabu mchangani kutokana na wasanii wengi kutamani kuwekewa kionjo cha kifaa hicho cha muziki.

King Maru-3

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents