Lady Jay DeePicha
Picha: Lady Jaydee ngangari licha ya safari ndefu ya kupanda Mt. Kilimanjaro
Leo ni siku ya nne ya safari ya Lady Jaydee na mume wake Gadner kuupanda Mlima Kilimanjaro. Kwa mujibu wa picha kutoka kwenye blog ya kilidovetour wanaiongoza safari hiyo, wote wanaonekana kuwa ngangari wasiokuwa na hata chembe moja ya kurudi nyuma.
Maendeleo ya safari yao:
January 8 – Mandara Hut(2700m) – Horombo Hut(3720m)
Masaa ya kutembea: 5
January 9: Acclimatization Day at Horombo Hut
Masaa ya kutembea: 4
January 10: Horombo Hut(3720m) – Kibo Hut(4703m)
Masaa ya kutembea: 5
Baadaye leo waanza safari ya kuelekea Uhuru Peak(5895m) kupitia Gillman’s point(5685m)
Hali zao kiafya
Gadner, Lady Jaydee na mpiga picha wao Justin wako fit na wana uwezo wa kuendelea hadi kituo kinachofuata.