Pre-Oder Infinix NOTE 11 kwa punguzo la Sh 50,000 na Ofa ya GB96 papo hapo

Habari njema kwa wapenzi wa simu za mkononi Infinix. Kampuni ya simu Infinix kupitia ukurasa wake wa @infinixmobiletz yatangaza rasmi punguzo la sh.50,000 kwa wateja watakaofanya malipo ya awali(pre-order) ya simu aina ya Infinix NOTE 11 https://www.infinixmobility.com/smartphone/note-11 kwa kutanguliza kiasi cha sh.50,000.

Infinix NOTE 11 itapatikana sokoni kuanzia tarehe 13 ya mwezi wa kumi na moja kwa bei ya sh.480,000 isipokuwa kwa wateja wa Pre-order kununua kwa bei ya punguzo ya kiasi cha sh.430,000. Vile vile mteja wa Pre-Order kuzawadiwa;
• Gaming earpods
• Smart band ya mkononi
• Powerbank
• GB96 za internet za mtandao wa Tigo.

Mfumo huu wa ulipiaji wa awali (Pre-Order) utafanyika kwa muda wa week moja na umeanza rasmi 5/11/2021 na utaisha rasmi 12/11/2021. Ambapo kwa mteja atayependezwa na huduma hii atafika katika maduka ya Infinix Smart Hub China Plaza na Infinix Smart Hub Mlimani City lakini pia huduma hii inapatikana maduka ya Tigo nchini kote.

Infinix NOTE 11 ilianza kuwa gumzo baada ya kuzinduliwa rasmi ugaibuni na hizi ndio baadhi ya sifa kuu:
• NOTE 11 simu ya kwanza kutoka toleo na NOTE kuja na AMOLED SCREEN ya nch 6.7FHD+ kioo chenye kunyonya chaji kwa asilimia ndogo zaidi kulinganisha na vioo vya simu nyengine za awali.
• NOTE 11 simu ya kwanza kutoka toleo na NOTE kuja na Wh33 ya kuchaji battery ya NOTE 11 yenye mAh 5000 baada ya nusu saa simu inajaa chaji kwa asilimia 75.
• NOTE 11 simu ya kwanza kwenye toleo la NOTE kuja na zoom lens 30X ya camera.

Kwa habari nyingi zaidi tafadhali wasiliana na Infinix kupitia 0717356468.

Related Articles

Back to top button