Burudani

Queen Darleen atoa maana tata ya ngoma yake ‘Nitakufilisi’

Msanii Queen Darleen amefunguka nini hasa amemaanisha katika ngoma yake mpya ‘Nitakufilisi’

First lady huyo wa label ya WCB amesema ngoma hiyo ni kwa ajili ya wanaume ingawa wengi hawataki kukubaliana na ukweli huo hasa pale wanapotoa fedha ili kuwapata wanawake.

“Wanaume wengi kwa asilimia kubwa wataniambia unatengeneza wimbo unatuumiza kweli, siwaumizi mimi najaribu kuwashtueni ninyi kwamba sisi tulivyo ndio tupo hivyo, mimi nawaimbia wanawake kwamba ninyi wanaume mnaliwa na sisi” amesema.

“Kwa hiyo kwa akili yako usiondoke kwamba umeondoka kulala na mimi umenila, kwa sababu umenipa hela” Queen Darleen ameiambia Magic Fm.

Wimbo huu mpya ‘Nitakufilisi’ ni ya tatu kwa Queen Darleen kutoa akiwa chini ya WCB baada ya ile kwanza ‘Kijuso’ na kolabo ambayo walifanya na wasanii wote wa WCB ‘Zilipendwa’.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents