Burudani

R. Kelly akana kunyanyasa wanawake

Muimbaji wa Marekani Robert Kelly maarufu kama R. Kelly amepinga tuhuma za unyanyasaji kwa wanawake zinazomkabili.

Kwa mujibu wa ripoti ya BuzzFeed News, iliyoandikwa na Jim DeRogatis ambaye kwa muda mrefu amekuwa akimfuatilia msanii huyo kwa maovu hayo. Ripoti hiyo pia inashirikisha washirika wa zamani wa Kelly, Cheryl Mack, Kitti Jones, na Asante McGee ambao wamerekodiwa wakiongea kuhusu uzoefu wao kwa nyota huyo wa muziki wa RnB.

Hata hivyo mwanasheria wa Kelly, Linda Mensch amesema kuwa mteja wake ameshtushwa na kukerwa na tuhuma hizo nzito na atahakikisha suala hilo analimaliza kwa uwezo wake wate na kusafisha jina lake.

“Mr. Robert Kelly is both alarmed and disturbed at the recent revelations attributed to him. Mr. Kelly unequivocally denies such allegations and will work diligently and forcibly to pursue his accusers and clear his name,” amesema mwanaseria huyo.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents