Habari

Rais wa Nigeria atoa neno kuhusu soko la watumwa Libya ‘Watu wangu wanauzwa kama mbuzi”

Rais wa Nigeria, Muhammadu Buhari amesema raia wote wa Nigeria ambao wamekwama Libya watarejeshwa nyumbani na kusaidiwa kurejelea maisha ya kawaida kwani nchini humo wamekuwa wakiuzwa kama Mbuzi.

Tokeo la picha la buhari
Muhammadu Buhari

Akizungumzia video za karibuni ambazo zimekuwa zikiwaonesha Waafrika wakiuzwa kwenye mnada wa watumwa nchini Libya, Rais Buhari amesema inasikitisha sana kuona “baadhi ya raia wangu wa Nigeria wanauzwa kama mbuzi kwa kiasi cha dola kadhaa nchini Libya”.

Ameonekana pia kushangaa iwapo raia wa Libya walijifunza lolote la maana tangu kuondolewa madarakani kwa Kanali Muammar Gaddafi mwaka 2011.

Walichojifunza pekee ni kuwapiga watu risasi na kuua. Hawakujifunza kuwa mafundi wa umeme, mafundi wa mabomba au ufundi wowote ule,” amesema Buhari.

Kwenye video iliyotolewa na CNN mapema mwezi huu, vijana kutoka mataifa ya Afrika kusini mwa jangwa la Sahara walionekana wakiuzwa kama wafanyakazi wa mashambani kwa wanunuzi.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Buhari ameapa kupunguza idadi ya raia wa Nigeria wanaolazimika kufunga safari ndefu na hatari kupitia jangwa la Sahara na bahari ya Mediterranean kufika Ulaya.

Chanzo : BBC

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents