Burudani

Mimi ni rasta man, mwiko kukata tamaa – Daz Baba

Msanii mkongwe wa muziki, Daz Baba ambaye aliwahi kufanya vizuri na wimbo ‘Namba 8’, amedai yeye ni rasta kwa hiyo ni mwiko kwake kukata tamaa katika maisha yake.

Rapa huyo wa zamani ambaye ngoma zake za sasa zimeshindwa kufanya vizuri, ameambia Bongo5 kuwa bado anaimani siku moja atafanya vizuri kama zamani.

“Mimi bado ni mkali sana, naamini hivyo na siku moja kila kitu kitaonekana,” alisema Daz Baba. “Mimi ni rasta na kwangu mwiko kukata tamaa najua siku moja mambo yatakuwa poa. Kama niliweza kufaka pale nilipofika kwa uwezo wa Mungu kwanini nishindwe wakati hata Mungu ametuambia tuwe wavumilivu,”

Rapa huyo alidai kitu ambacho kinamfelisha na kushindwe kufanya vizuri ni management ambayo itamsaidia kumuongoza na kuusimamia muziki wake.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents