Burudani

Natukanwa kisa kumuunga mkono Rais Magufuli – Mrisho Mpoto

Msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto amedai toka aonyeshe nia yake ya kumuunga mkono Rais John Pombe Magufuli amekuwa akitukanwa pamoja na kutupiwa maneno ya kejeli.

                              Mrisho Mpoto akiwa na Rais Magufuli
Muimbaji huyo ambaye ni mmoja kati ya wasanii ambao wanafanya show nyingi za Ikulu toka Rais huyo aapishwe, amesema yeye ataendelea kumuunga mkono Rais huyo kwa kuwa ni kiongozi ambaye anawapigania wananchi wa chini.

“Nimepokea matusi mengi, kebehi, na maneno machafu juu ya mimi kuunga mkono utendaji wa Rais Magufuli, kitu ambacho nakiamini kuna “KUKUBALIANA KWA KUTOKUBALINA” lakini siyo kumtukana mtu mwingie siyo busara hata kidogo, kwa kuwa tu hakusema au hakufanya ambacho nafsi yako ilipenda kusikia,” aliandika Mpoto Instagram.

“Kilichonifanya niandike ujumbe huu ni kuwa nisiwekewe maneno mdomoni yakua nimesema Rais Magufuli ni Mungu, kwa wale ambao hawakuangalia sherehe za MEI MOSI jana, naomba niseme kuwa hayo maneno siyo kweli na yamebadilishwa kutoka kwenye ukweli wa niliosema, Mimi ni mtu mwenye hofu na Mungu siwezi kusema hivyo,” aliongeza.

Mpoto amedai imekuwa ni tamaduni wa baadhi ya watu kuwashambulia watu ambao wameonyesha nia ya kumsupport Rais Magufuli.

“Kumekuwa na utamaduni ikitokea mtu anauunga mkono utendaji wa Rais kuna ibukuka kundi la wapinga maendeleo na kuanza kutukana. Naomba ijulikane kuwa sababu za kumunga mkono Rais, yale niliyokua nayaongea huko nyuma naona yanafanyiwa kazi hivi sasa!! MRISHO MPOTO mpaka sasa namuunga mkono Rais MAGUFULI, Iwe nachumia tumnbo kama inavyosemwa au nimevimbilwa kwa shibe,” alisema Mpoto.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents