Habari

RC Ayoub awashukuru wananchi wake kwa ukarimu na ushirikiano

Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Ayoubu Mohamed Mahmoud amewashukuru wakazi wa Mkoa huo kwa ushirikiano walioonesha katika kipindi chote cha maandalzi ya kuadhimisha kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru na kumbukumbu ya kifo cha Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambaraga Nyerere.

Akiongea na waandishi wa habari, RC Ayoub ameeleza kuwa amefarijika kwa ushirikiano na umoja walioonesha kabla na baada sherehe hizo, ambazo zimeingia katika historia ya kufanyika kwa mara ya kwanza kufanyika Zanzibar.

RC Ayoub pia alisisitiza hata omba radhi kwa wale ambao aliwakazwa kwa kuwa alikuwa akitiza wajibu wake katika kuhakikisha anafanikisha shughuli hizo, bali anaomba radha kwa wale aliowakwanza bila kukusudia.

Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru zilifanyika siku ya Jumamosi hii tarehe 14 mwezi wa kumi, ambapo kilele cha mbio hizo zilienda sanjari na maadhimisho ya kumbukumbu ya kifo cha Mwalimu Julius Kambaraga Nyerere na Wiki ya Vijana.

Vile vile viongozi mbalimbali wa serikali kutoka Bara na Visiwani waliudhuria sherehe hizo ambazo mgeni rasmi akiwa ni Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents