Habari

RC Chalamila apiga marufuku malori kupaki ‘service road’

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe Albert Chalamila amesema hayo leo Januari 05, 2024 alipofanya ziara ya kukagua maeneo ya service Road Barabara ya Uhasibu-Kurasini Jijini humo.

RC Chalamila amesema kila mwenye ICD ni lazima awe na sehemu ya kupaki malori yake na sio vinginevyo “Service road ni kwa ajili ya matumizi ya Umma sio mwenye malori kupaki malori yake” Amesema Chalamila

Aidha RC Chalamila amesema leo Februari 06, 2024 saa 2:00 Asubuhi atafanya kikao na wamiliki wote wa ICD, TANROAD na Jeshi la Polisi wanaohusika na Usalama barabarani kwa lengo la kufikia muafaka wa upakiji hovyo wa malori katika Jiji “tutatoa muda service Road zote ziwe wazi hakuna malori kupaki tena” Alisisitiza RC Chalamila

Vilevile RC Chalamila alifika kurasini kwa lengo la kutatua Changamoto ya magari kuingia ofisi za Baraza la Maaskofu Tanzania Kurasini ambapo ameuhakishia uongozi wa baraza hilo kutatua Changamoto hiyo mapema iwezekanavyo, hata hivyo tayari TANROAD wamewasilisha mpango wa muda mfupi wa kutatua Changamoto hiyo na mpango wa muda mrefu ukiendelea

Naye Mtaalaam kutoka TANROAD Clever Akilimali amesema Taasisi yao imeendelea kutoa elimu kwa umma juu ya matumizi sahihi ya “Service road” na imekuwa ikitenga maeneo kwa ajili ya kupaki malori kama vile kibanda cha mkaa na kibamba na maeneo mengine rai yake ni kila mmiliki wa Lori na wenye ICD kuacha kupaki malori kwenye service Road ili kutoa fursa kwa matumizi yaliyokusudiwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents