Habari

RC Makonda akagua ujenzi wa jengo la dharura hospitali ya Temeke

Mara baada ya ukaguzi Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ameeleza kuridhishwa na hatua za ujenzi huo wa jengo la huduma za dharura na kwamba kukamilika kwa ujenzi huo mwishoni watahamia katika Wilaya za Ilala na Kinondoni.

Kwamujibu wa mkandarasi Abdulkadir Msangi amesema mpka sasa hatua za ujenzi umekamilika kwa asilimia 85% na kwamba litakamilika kabla ya Mwezi Desemba.

Kwa upande wa Mganga mkuu Hospitali ya Temeke Amani Malima amesema kukamilika kwa jengo hilo kutasaidia huduma za dharura kuptikana kwa huduma hiyo kwa haraka badala ya kuwapeleka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kama ilivyosasa, ambapo mpaka sasa hospitali hiyo inapokea wagonjwa 2000 kwa siku na miongoni mwao Wagonjwa 200 huwa wanahitaji huduma za dharura.

Ujenzi huo unaodhaminiwa na Ubalozi wa Japani nchini Tanzania umegharimu shilingi milioni 323.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents