Habari

RC Makonda atengua kauli ya DC Ilala ya kukataza watu kuabudu siku za wiki ‘Mimi mwenyewe mlokole hunipangii muda wa kusali’

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, ametengua kauli ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Bi. Sophia Mjema, ya kuwazuia watu kuabudu siku za juma.

Image result for rc makonda
RC Makonda

RC Makonda amesema hawezi kuwapangia watu masaa na siku za kumuabudu Mungu wao wanayemuamini na kuwataka watu wa wilaya hiyo waabudu kwa kufuata utaratibu uliowekwa.

Serikali haina dini, Natengua kauli ya Mkuu wa Wilaya ya Ilala, watu wendelee kwa imani zao bila kuathiri sheria za nchi, viongozi tunapaswa kuwa makini tunapoingia kwenyeatika mambo ya dini, mambo ya dini ni mambo imani, mimi mwenyewe hapa ni mlokole hunipangii muda wa kusali,” Amesema Makonda leo Oktoba 22, 2019 kwenye mkutano wake na Waandishi wa Habari.

Siku za hivi karibuni DC Mjema alisikika akihutubia wananchi na kusema kuwa anatambua siku za kusali ni tatu tu na kuhoji watu wanaosali siku za kawaida wanafanya kazi muda gani.

Kuna watu wanapiga mapambio Jumatatu mpaka Jumatatu, Ukiingia huko ndani watu 5, wewe Jumatatu mpaka Jumatatu unaita watu, huna watu funga. Sisi tunajua katika kuomba ni mara hizi tatu. Yaani Ijumaa (Waislam), Jumamosi (Wasabato) na Jumapili (Wakristo wengine). Hizi siku nyingine hakuna marufuku, Ninyi kazi mnafanya saa ngapi, Jumatatu hadi Jumatatu?,” Alikemea DC Mjema.

https://www.instagram.com/p/B36mOKXhvSn/

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents