Burudani

Reputation ya Taylor Swift yatisha kwa mauzo ya awali

Ifikapo Novemba 10 mwaka huu, mwanadada Taylor Swift anatarajia kuachia albamu yake ya ‘Reputation’ ambayo mpaka sasa imeshafikisha mauzo ya kopi 400,000 ikiwa bado haijatinga sokoni.

Kupitia albamu hiyo ngoma kama “Look What You Made Me Do” na “…Ready for It?” zimesha toka na zimefanikiwa kuwepo katika chati kadhaa za muziki ikiwemo ya Billbord.

Hii si mara ya kwanza kuwa msanii huyo kuuza kopi nyingi kwa muda mfupi kwani amesha wahi kuuza kopi milioni moja ndani ya wiki ya kwanza kwa albamu kama ‘1989′ iliyotoka mwaka 2014, pia albamu ya ‘Red’ iliyotoka 2012 na ‘Speak Now’ ya mwaka 2010.

Albamu ya ‘Reputation’ ni ya sita kwa msanii huyo katika maisha yake ya kimuziki na mazuo ya kopi hizo yanahusisha U.S.A pekee hiyo Swift anauzo wa kuuza kopi nyingi zaidi punde tu albamu hiyo ikiingia sokoni.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents