Michezo

Rhulani Mokwena aipania Robo Fainal Klabu Bingwa Afrika (CAF)

Kocha mkuu wa Mamelodi Sundowns, Rhulani Mokwena anasema ni muhimu kwa klabu kabambe kama Mamelodi Sundowns kuwa mara kwa mara katika awamu ya mashindano ya TotalEnergies CAF Champions League.

Mokwena, ambaye alikuwa msaidizi wa Pitso Mosimane wakati timu hiyo ya Afrika Kusini iliponyanyua taji lake la kwanza la bara mwaka 2016 amefanikiwa kutwaa kijiti hicho na kuiongoza timu hiyo kuwa miongoni mwa bora zaidi barani humo.

Wakati klabu kutoka mji mkuu wa taifa hilo ilifurahia mafanikio makubwa katika uzinduzi wa Ligi ya Soka ya Afrika, klabu hiyo bado inauguza jeraha la kupoteza msimu uliopita wa nusu fainali dhidi ya Wydad AC ya Morocco katika msimu ambao walionekana kutozuilika.

 

Mokwena alisema ili klabu hiyo iweze kutwaa tena Ligi ya Mabingwa ya CAF ya TotalEnergies, jambo ambalo anaamini litafanyika, ni lazima Sundowns wawe kwenye hatua ya mtoano mfululizo.

“Itachukua uthabiti mwingi, bidii na bahati nyingi. Unahitaji bahati kidogo. Ukiangalia AFCON na mashindano hayo ya kiwango cha juu, hakuna tofauti kubwa. Nadhani ukiangalia Ivory Coast na jinsi walivyoshinda AFCON, walikuwa wametoka, wakarudi na hatimaye wakashinda,” alisema Mokwena.

Mtaalamu huyo, ambaye ndio kwanza amefikisha umri wa miaka 37 mwezi Januari pia aliongeza kuwa ni muhimu kwa klabu hiyo kuendelea kuwa katika awamu ya mtoano ya kinyang’anyiro hicho kwani ndivyo washindani wa taji hufanya mara kwa mara katika kila msimu.

“Lazima uwe humo ndani. Unatakiwa kuingia robo fainali. Unapaswa kuwa katika nusu fainali. Lazima uwe kwenye fainali. Ukiwa hapo, unaweza basi kuota kwenda mbali zaidi. Unaweza kuhisi haja ya kunyoosha mbawa zako na kujaribu kupaa juu kidogo kuliko uliyo nayo. Ingawa ni kazi ngumu kama inavyoweza kuonekana na kusikika, ni jambo ambalo linawezekana, lakini lazima uende mchezo mmoja baada ya mwingine kisha natumai miungu ya soka itakutabasamu” alimalizia Mokwena.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Imeandikwa na Mbanga B.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents