Burudani

Rhymes Biashara kuja na wimbo ‘Fefea’ baada ya kufanya vizuri na wimbo ‘Silolo’ akiwa Raymond

Msanii wa muziki Rhymes Biashara ajipanga kuachia wimbo wake mpya ‘Fefea’ baada ya kufanya vizuri na wimbo ‘Silolo’ akiwa amemshirikisha Raymond aka Rayvanny.
daimond-x-rayvanny

Muimbaji huyo ambaye alikuwa Tip Top kipindi cha nyuma, amesema tayari ameshafanya maandalizi audio pamoja na video ya wimbo huo ila anasubiria timing ya kuachia kazi hiyo.

“Nashukuru Mungu ‘Fefea’ imekamilika, Abby Dady amesimama kwenye audio na video nimefanya na Pablo. Kwa hiyo kikubwa naomba mashabiki wangu wanipokee kwa mikono miwili,” alisema Rhymes.

Muimbaji huyo alisema jina la wimbo ‘Fefea’ maana yake ni Cheza, na video imeandaliwa mkoani Njombe.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents