HabariMichezo

Ronaldo alitaka kuondoka Qatar

Inadaiwa kuwa Staa wa Ureno, Cristiano Ronaldo alitaka kupakia mabegi yake na kuondoka nchini Qatar baada ya kukasirishwa kutokana na kutopangwa kwenye kikosi cha kwanza katika mechi dhidi ya Uswizi.

Kocha wa Ureno, Fernando Santos amekuwa kwenye presha kubwa ya kumuanzisha Ronaldo ndani ya timu ya taifa licha ya kuonekana kama kiwango chake kimeshuka ukilinganisha na wachezaji damu changa waliopo kikosini.

Mchezaji huyo wa zamani wa Man United ameonekana kama vile ameingia kwenye mvutano na bosi wa kikosi hicho kutokana na mitazamo yake binafsi.

Kwa mujibu wa daily mail, Ronaldo alitaka kupakia kila kilichochake na kutimka Qatar baada ya kufanya mazungumzo na kocha Santos na kubaini asingekuwepo ndani ya kikosi kiilichocheza mechi ya hatua ya 16 bora wiki hii.

Baada ya mchezo huo Ronaldo alikaa chini na Santos na kumuweka wazi kuwa hakufurahishwa na uamuzi wake wa kutomchezesha – akitishia kuondoka Qatar.

Hata hivyo inadaiwa staa huyo alijirudi kutokana na kutambua umuhimu wake ndani ya kambi ya timu ya taifa na kubadili mawazo ya kuondoka.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents