Burudani

Rosa Ree awafungukia wasanii wanaonunua views YouTube (+video)

Rapper Rosa Ree amefunguka mambo kadhaa kuhusu idadi ya views katika mtandao wa YouTube kutumika kama kigezo cha muziki kukubalika.

“Kuna watu wanaosikiliza muziki na kuupenda na kuukubali lakini hawana access ya YouTube, so many wanaweza kusikiliza hata wabibi kijijini wanasikiliza huo wimbo lakini hawana uwezo wa kuingia YouTube, so huwezi ukasema views za YouTube ndio uzuri wa wimbo au ndio ukubwa na kukubalika” amesema Rosa Ree.

Alipoulizwa iwapo anaamini kuwa kuna tabia ya wasanii kununua views kama inavyokuwa ikidaiwa, alijibu; “sijui kama inawezekana kwa hiyo hicho kitu siwezi kukiongelea kitu ambacho sikijui, mimi personal sijawahi kununua views”.

Kwa sasa Rosa Ree anafanya vizuri na ngoma yake mpya ‘Dow ‘ baada ya kukimbiza na ngoma kama Up In The Air na One Time.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents