Michezo

Serengeti Boys yapata ushindi dhidi ya vijana wenzao wa Burundi

Timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys imepata ushindi wa 3-0 dhidi ya Burundi jana katika Uwanja wa Kaitaba, Bukoba katika mchezo wa kirafiki wa kujiandaa na fainali za vijana Afrika Mei mwaka huu nchini Gabon.
Mchezo huo uliochezeshwa na refa Mtanzania, mwenye beji ya FIFA, Deonisya Rukyaa.

Mabao ya vijana wa Tanzania yalifungwa na kiungo Muhsin Makame na beki wa kushoto, Nickson Kibabage aliyepanda kusaidia mashambulizi.

Makame alifunga dakika ya 19 akimalizia pasi ya Israel Mwenda kutoka upande wa kulia, wakati Kibabage alifunga dakika ya 38 baada ya kupanda na mpira upande wa kushoto na kuingia nao ndani kabla ya kumtungua kipa Djuma Bitiyaweho.

Pamoja na wenyeji kurudi vyumba vya kubadilishia nguo wakiwa wanaongoza kwa mabao 2-0, lakini timu hizo zilishambuliana kwa zamu na ila uimara wa safu ya ulinzi ya Tanzania iliwafanya Burundi wasipate hata goli moja, bao la tatu, lililofungwa na Nahodha Kevin Nashon Naftali dakika ya 72.

Timu hizo zitarudiana Jumamosi Uwanja wa Kaitaba, kabla ya Serengeti kupanda ndege kwenda Dar es Salaam kucheza na U-17 ya Ghana Jumatatu.

Related Articles

Check Also
Close
Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents