Habari

Serikali itaendelea kulinda uhuru wa kuabudu – Majaliwa

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema serikali itaendelea kulinda uhuru wa kuabudu kwa kila Mtanzania na haitamvumilia mtu wala kikundi chochote kitakachofanya mambo yanayotishia usalama na amani ya nchi.

Majaliwa aliyasema hayo Jumatatu hii alipozungumza katika Baraza la Maulid ya kumbukizi ya kuzaliwa Mtume Muhammad (S.A.W) lililofanyika kitaifa kijijini Shelui wilayani Iramba, mkoani Singida.

“Serikali itaendelea kulinda uhuru wa kila mwananchi kuabudu kile anachoona kinafaa. Serikali itafanya kila liwezekanalo kusimamia na kuhakikisha hakuna kikundi kinahatarisha usalama wa nchi na hatutayumba katika hilo,” alisema Majaliwa.

“Mara nyingi huwa napenda kurejea kauli ya Baba wa Taifa (Mwalimu Julius Nyerere) aliyosema kuwa ‘Nchi haina dini bali watu wake wana dini’ na kusimamia hilo kwamba tutaendelea kuwezesha uhuru wa kuabudu.”

Maulid ilisomwa juzi usiku na mapumziko pamoja na Baraza la Maulid ilikuwa jana.

BY: EMMY MWAIPOPO

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents