Habari

Serikali yatoa neno kuhusu tuhuma za kutekwa Mdude Chadema, yataka Mchungaji Msigwa ahojiwe na Polisi (+video)

Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, imesikitishwa na taarifa zinazosambaa za kupotea kwa kada wa CHADEMA, Mdude Chadema na kueleza kuwa Jeshi la polisi lipo kwenye upelelezi wa tukio hilo.

Akijibu swali la Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa aliyedai kuwa kijana huyo katekwa, Naibu Waziri Mambo ya Ndani ya Nchi Eng. Hamad Massauni ameliagiza Jeshi la Polisi kumtafuta Mbunge wa Iringa mjini Pater Msigwa ili awasaidie kupata taarifa za kupotea kwa kijana huyo, hii ni baada ya Msigwa kulieleza Bunge kuwa Mdude Chadema hajapotea bali ametekwa.

Related Articles

Back to top button

Adblock Detected

Please don't block our ads, we rely on these ads to serve you with credible contents